Friday, June 15, 2012

DANNY MRWANDA AIGEUKA YANGA, AHAMIA SIMBA!

.
MAKAMU Mwenyekiti wa mabingwa wa Tanzania Simba SC Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema club hiyo imekamilisha usajili wao kwa kukinasa kifaa kimoja kikali ambacho Yanga walikuwa wanakiwania.
Ingawa Kaburu hakutaka kutaja jina la mchezaji huyo, lakini uchunguzi wa BIN ZUBEIRY umebaini kwamba, mchezaji mwenyewe ni mshambuliaji wa Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Davis Mrwanda ambaye kweli Yanga walikuwa wanamtaka wakashindwana.
BIN ZUBEIRY inajua Mrwanda aliyewahi kuchezea Simba kabla ya kwenda ughaibuni, atasaini Simba SC wakati wowote kwa sababu mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanaendelea vizuri.
Mkataba ambao atasaini Mrwanda ni ambao utamruhusu kuondoka wakati wowote atakapopata timu nje ya Tanzania.
Pamoja na ishu ya Mrwanda, Kaburu alisema kwamba mchezaji anayefunga usajili wa Simba ni beki wa kati wa kigeni, ambaye bado wanafuatilia uwezo wake ili kujiridhisha.

Lakini Kaburu amesema mahitaji yote ya Simba yametimia, kwa kusajili winga Kiggi Makassy, washambuliaji Abdallah Juma, Mrwanda, viungo Ibrahim Jeba, Patrick  
Mbivayanga, Salim Kinje, Mussa Mudde, beki wa kushoto, Paul Ngalema na kupandisha wachezaji watatu wa U-20.
Aidha, Kaburu alisema ili kuboresha zaidi kikosi, wanafikiria kusajili beki wa kulia kwa sababu Nassor Masoud ‘Chollo’ ni majeruhi wa muda mrefu na kuna uwezekano bahati ikamuangukia beki wa timu hiyo aliyekuwa akicheza kwa mkopo Villa Squad, Haruna Shamte.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Kiggi Makassy ameripoti rasmi kazini, kwa mwajiri wake mpya Simba SC na kuanza mazoezi leo asubuhi. “Kiggi ameanza mazoezi rasmi leo,”alisema Kaburu kuhusu kiungo huyo waliyemuiba kwa watani wao wa jadi, Yanga SC.  (Stori yote imeandikwa na Bin Zubery wa bongostaz.blogspot.com)

NDOA YA H-BABA, FROLA UTATA


Ndoa ya nyota wanaotamba kupitia fani ya muziki na filamu Bongo, Hamis Ramadhan Baba, ‘ H-Baba’ na Frola Mvungi, bado iko gizani kufuatia, kijana huyo kushindwa kufikia uamuzi.


Akizungumza ‘live’ na mtandao namba moja kwa stori za mastaa (Teentz.com) H-Baba amesema kuwa hana uhakika kama jambo hilo linaweza kupewa nafasi hivi sasa kwa kuwa kuna mambo mengi yanyomfanya kushindwa kufikia uamuzi wa kufunga ndoa na mwigizaji huyo

“Bado kuna utata, sijafikia uamuzi wa kufanya jambo hilo hivi sasa, sitaki kusema sana kwa sababu najua kuna watu ambao wanajaribu kuingilia uhusiano huu, ki ukweli sijafikia uamuzi kuna mambo madogo madogo bado nayachunguza kwa mwenzangu na wakati ukiwadia basi kila kitu kitakuwa wazi” alisema H-Baba aliyeingia kwenye uhusiano na Frola mwaka mmoja uliopita.

Wednesday, June 13, 2012

MHABARISHAJI WA MTANDAO HUU AFUNGA NDOA YA KIFAHARI.

                                                                      Joseph Philbert
Mwanahabari wa kujitegemea kupitia mtandao wa kijamii wa "josephtele.blogspot.com" ameamua kuachana na maisha ya kibachela na kuamua kuoa. Ndoa hiyo ya kifahari ilfungwa tarehe 2 mwezi Februari mwaka huu na kufuatia na sherehe kubwa katika ukumbi wa kambi ya jeshi Lugalo.Pongezi kwake na kila kheri katika maisha mapya aliyoyaanza.

                                          Wanafunzi wa chuo cha Tumaini Dar ambao wanasoma                                  darasa moja na bwana harusi wakiwa katika 
pichamoja na maharusi baada ya kukabidhi.

                                           kampani ya bwana na bibi harusi wakichukua chakula

                                      Bwn. harusi Joseph Philbert na mkewe Bi. Consolatha Charles.